Mabingwa wa ligi ya NBC Premier League Yanga SC ndio timu pekee iliyomaliza ligi kwenye msimu wa 2021-2022 barani Afrika pasipo kupoteza mchezo wowote kwenye michezo 30 waliyocheza msimu mzima.

Yanga SC kwenye michezo 30 wamefanikiwa kushinda michezo 22, na kutoa sare michezo 8, huku wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja mpaka wanafanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania.

Yanga SC

Yanga SC kwenye msimu 2021-22 mechi walizoshinda ushindi mkubwa ni mbili tu dhidi ya Mbeya Kwanza FC na Dodoma jiji ambapo waliwatwanga goli nne kila mmoja. Pia walitoka sare ya kutokufungana kwenye michezo mitano tu.


Yanga SC kwa sasa inajianda na mchezo wa fainali ya AZAM Confideration Cup siku ya Jumamosi ya tarehe 2-7-2022 kwenye uwanja wa Sheikh amri abeid jijini arusha dhidi ya Coastal Union FC.

Coastal Union FC anaweza kuiharibu furaha ya wanajangwani kwa kuwafunga kwenye mchezo wa fainaili hiyo?


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa