Mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Congo Yannick Bangala leo ameongeza kandarasi yake ya kuitumikia klabu ya Yanga SC hadi mwaka 2024 na kukata mzizi wa fitina kuhusu hatma yake kwenye klabu hiyo.

Yannick Bangala Litombo alisajiriwa na klabu ya Yanga mwaka 2021 akitokea klabu ya nchini kwao Congo Motema Pembe ambayo nayo ailitumikia kwa miaka mitano akitokea klabu ya FC Les Stars.

Yannick Bangala, Yannick Bangala Kuendelea Kuwa Kijani na Njano Hadi 2024, Meridianbet

Yannick Bangala Litombo amefanikiwa kuichezea timu yake ya taifa Congo michezo 27, tangu alipoitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu hiyo, wakati akiitumikia klabu ya Motema Pembe.

Pia ukiachana na Kandarasi ya Bangala, klabu ya Yanga pia leo imetangaza kuwa siku ya Jumatatu Agosti 1 watafungua rasmi wiki ya mwananchi, huku kamati ya maandalizi ikiwa inaongozwa na raisi wa klabu hiyo Eng Hersi akiwa na wajumbe sita kwenye kamati hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa