Klabu ya Arsenal imemsainisha Leo Messo, mtoto mwenye miaka 10 katika academy ya timu hiyo. Mtoto huyo Raia wa Kenya anadaiwa kuwa na kipaji kikubwa sana.
Mtoto huyo anatajwa kuwa na kipaji cha hali ya juu akiwa ameanzia katika Klabu ya West Ham United kabla ya kusainishwa na Arsenal ambapo amepokelewa na kocha wa academy hiyo Per Mertesacker.
Arsenal imekuwa na historia ya kuzalisha wachezaji wakubwa wenye asili ya Afrika kupitia academy, baadhi yao wakiwa ni Chuba Akpom, Alex Iwobi, Eddie Nketiah na Bukayo Saka.
Kumekuwa na tabia ya timu za Uingereza kusainisha watoto katika akademi zao na kisha kuwaandaa na kuwatumia katika timu kubwa na huwa wanafany vitu vikubwa sana. Leo Messo kama anavyoitwa kijana huyo anatarajiwa kuja kuleta mabadiliko makubwa katika soka baadae.
Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.
Magdalena
Wana malengo nae makubwa
Sauda
Tisha dogo