Zinedine Zidane amefunguka juu ya tetesi zikimuhusisha Mohamed Salah na Real Madrid kuelekea mchezo wa robo fainali ya Champions League dhidi ya Liverpool.

Zidane Avunja Ukimya Juu ya Salah Kutua Real Madrid

Salah amekuwa katika vichwa vya habari wiki iliyopita baada ya kukiri kwamba yupo tayari kucheza nchini Spain hapo baadaye.

Mshambuliaji huyo wa The Reds kwasasa anajaribu kuonesha hisia zake za kuhama na kwenda huko Santiago Bernabeuwakati wa majira ya joto, Lakini Zidane amepuuza kuhusishwa na kumuhitaji mchezaji huyo wa miaka 28 wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Aliulizwa kama angependa kumfundisha Salah, bosi huyo wa Real Madrid aliwaambia maripota: “Siyo mchezaji wangu.

“Nina wachezaji 25 hapa kwa sasa mimi ni kocha wa Real Madrid na ninafurahia kila siku ya matukio.

Salah aliongeza ukubwa wa uvumi juu ya hatima yake huko Liverpool wakati wa mahojiano na chapisho la Hispania AS mwezi Desemba baada ya kusema anahitaji changamoto mpya katika ligi ya LaLiga.

“Nadhani Barcelona na Real Madrid ni vilabu vikubwa, nani anayejua kuwa nini kitatokea hapo baadaye,” Alisema.

Salah alijiunga na Liverpool mwaka 2017 kwa kitita cha £37m ($51m) akitokea Roma wakati wa dirisha la majira ya joto.

Mmisri huyo amefunga mabao 120 katika michezo 193 tangu ajiunge na Reds akisaidia kutwaa taji la Premier League na Champions League.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

Zidane, Zidane Avunja Ukimya Juu ya Salah Kutua Real Madrid, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa