Mkurugenzi wa Borussia Dortmund, Michael Zorc amesisitiza kwamba Erling Braut Haaland ataendelea kuwepo klabuni hapo katika msimu wa usajili wa kiangazi hata kamani watakosa nafasi katika nne bora za Bundesliga.

Haaland alikosa penati dhidi ya Union Berlin Jumatano jioni, lakini walishinda kwa 2-0 na kusonga mbele kwa alama 52, alama nne nyuma ya Eintracht Frankfurt anayeshika nafasi ya nne katika Bundesliga.

Kumekuwa na maoni kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway anaweza kulazimisha kuondoka katika soko lijalo ikiwa hawatashiriki ligi ya Mabingwa Uropa.

Lakini, Zorc amesema kuwa mshambuliaji huyo atabaki na Dortmund bila kujali nafasi yao kwenye kwenye msimamo wa ligi.

Zorc -Haijalishi, Haaland Atasalia Dortmund

“Haijalishi tunaishia wapi, Erling Haaland ataendelea kucheza nasi,” Zorc aliiambia Sky Deutschland.

Kijana huyo wa miaka 20 amekuwa katika fomu bora akiwa na BVB msimu huu wa 2020-21, akifunga mabao 35 na kusajili assist 11 katika mechi 37 kwenye mashindano yote.

Manchester United, Manchester City, Liverpool, Chelsea, Real Madrid na Barcelona wote wanadaiwa kutaka kumsajili fowadi huyo katika soko lijalo.


 

MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

Haaland, Zorc -Haijalishi, Haaland Atasalia Dortmund, Meridianbet

CHEZA HAPA

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa