Klabu ya soka ya Arsenal kutoka Uingereza imethibitisha kumpa mkataba ulioboreshwa rasmi mlinda mlango wao namba moja, David Raya, utakaodumu hadi mwezi Juni mwaka 2028. Hatua hii ni sehemu ya mkakati wa klabu hiyo kuhakikisha kuwa nyota wake muhimu anabaki klabuni kwa muda mrefu.
Taarifa zinaeleza kuwa makubaliano ya awali yalifikiwa tangu dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi, lakini sasa Raya amesaini rasmi mkataba huo huku akipokea ongezeko la mshahara kama ilivyopangwa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Katika rekodi ya Kidunia, David Raya anachukuliwa kama mmoja wa walinda mlango bora. Huku akiendelea kuwa tegemeo la Arsenal katika mechi kubwa, akionyesha uwezo wa hali ya juu katika kudhibiti mashambulizi na kuongoza safu ya ulinzi.