Mshahara wa Cristiano Ronaldo Al-Nassr ni Kufuru | Kwa Siku Kulipwa TZS 1.3B

Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo ni rasmi amejiunga na klabu ya Al-Nassr ya nchini Saudi Arabia kwa mkataba wa miaka miwili ambao utadumu mpaka mwaka 2025 wenye thamani ya Bilioni 492.

 

Ronaldo

Klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Saudia ilimtambulisha rasmi Ronaldo, ambapo walisema kuwa usajili huo ni kwaajili ya kuinua soka la nchi hiyo.

“Hii ni zaidi ya historia kuwekwa, huu ni usajili utakaovutia mafanikio makubwa kwa klabu yetu, na kuvutia pia mafanikio kwenye Ligi, Taifa na vizazi vijavyo, vijana wa kike na kiume kuwa bora. Karibu Cristiano Ronaldo kwenye nyumba yako mpya” -Al-Nassr FC

Na sasa tupige mahesabu kidogo tu hapa kuhusiana na mshahara atakaokuwa anavuta mwamba huyo, ambaye ameaga rasmi soka la ushindani ngazi ya vilabu baada ya kutemwa na Manchester United kutokana na mahojiano aliyoyafanya na Morgan Piers yaliyoishutumu klabu hiyo kumsaliti.

Kwa Mwaka mmoja = Bilion 492 TZS
Kwa mwezi mmoja= Bilion 41 TZS
Kwa Siku moja = Bilion 1.3 TZS
Kwa Saa moja = Milion 554 TZS
Kwa dakika moja = Milion 9 TZS
Kwa Sekunde moja = 150k TZS

Inamaanisha kwamba kila sekunde atakayo akiingia uwanjani atalipwa mshahara wenye kiasi cha Laki moja na Elfu Hamsini.

Mkataba wa Ronaldo utajumuisha gharama za matangazo kibiashara atakazokuwa anaingiza kipindi chote cha mkataba wake na Al-Nassr.

Acha ujumbe