GAMONDI ATOA MSIMAMO MKALI

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hawafikirii ushindi kwenye mechi za kirafiki hivyo kupata ushindi ni matokeo ambayo yanawaongezea nguvu kuendelea kupambana zaidi.

Ipo wazi kuwa Yanga imeweka kambi Afrika Kusini kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25 unaotarajiwa kuanza Agosti 8 2024.

Julai 24 2024 Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TS Galaxy kwenye mchezo uliochezwa Afrika Kusini na bao pekee la ushindi lilifungwa na Prince Dube dakika ya 55 ikiwa ni bao lake la kwanza kwenye mechi za ushindani baada ya kutambulishwa kuwa mali ya timu hiyo.

Gamondi amesema: “Hatufikirii sana ushindi kwenye mechi ambazo tunacheza hasa katika maandalizi ya msimu mpya kikubwa ni kuona kwamba kile ambacho tunajifunza kinafanyiwa kazi kwa umakini.”.

Mabingwa hao wa msimu wa 2023/24 wanatarajiwa kucheza mchezo wa Ngao wa Jamii Agosti 8 dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa.

Acha ujumbe