Bodi ya Ligi Kuu Tanzania TPLB imetangaza rasmi mabadiliko ya uwanja wa mchezo namba 169 wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026, utakaozikutanisha klabu kongwe za Simba SC na Yanga sc, maarufu kama Kariakoo Derby.
Awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, lakini sasa utafanyika katika Uwanja wa Mej. Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni jijini Dar es Salaam. huku mynama Simba akiwa mwenyeji wa pambano hilo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, pambano hilo linatarajiwa kupigwa Mei 3, 2026 kuanzia saa 12:00 jioni, huku mashabiki wakitarajiwa kushuhudia ushindani mkubwa kama ilivyo desturi ya dabi hiyo.
Sababu ya mabadiliko hayo ni kuendelea kwa matengenezo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, hali iliyolazimisha TPLB kuchukua uamuzi wa kuhamishia mchezo huo katika uwanja mwingine.
TPLB imethibitisha kuwa klabu za Simba na Yanga pamoja na wadau wote wa Ligi Kuu ya NBC wamejulishwa mabadiliko hayo, huku maandalizi yakianza mara moja ili kuhakikisha mchezo unafanyika kwa kiwango cha juu kinachoendana na hadhi ya ligi hiyo barani Afrika.

