Klabu ya Simba SC pamoja na TRA United zote mbili zimepigwa faini ya Shilingi milioni 5 kila moja kutokana na tukio la vurugu lililohusisha walinzi wa klabu hizo (stewards) baada ya timu hizo kuwasili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Stadium, mkoani Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, vurugu hizo zilihusisha kupigana kwa walinzi wa pande zote mbili Simba na TRA mara baada ya timu kuwasili uwanjani, jambo lililokiuka kanuni za udhibiti za mashindano. Adhabu hiyo imetolewa chini ya Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika tukio jingine, Simba SC wamepigwa faini ya ziada ya Shilingi milioni 10 baada ya mashabiki wao kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili wa mchezo, kufuatia uamuzi wa kuashiria mchezaji wa Simba kuotea wakati wa mchezo.
Tukio hilo limeelezwa kuwa ni kosa la kurudia, kwani mashabiki wa Simba wamewahi kufanya vitendo kama hivyo katika michezo miwili tofauti msimu huu wa NBC Premier League 2025/2026, hali iliyochangia adhabu kali zaidi kwa klabu hiyo.
Mamlaka za ligi zimesisitiza kuwa hatua hizo zinatokana na Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu, zikiwa na lengo la kudhibiti nidhamu na kuhakikisha mazingira salama ya michezo. Wito umetolewa kwa klabu zote kuheshimu sheria na kudhibiti mashabiki pamoja na watendaji wao ili kuepuka adhabu zinazoweza kuathiri ushindani wa ligi.

