Kocha wa Chelsea, Liam Rosenior, amesema bado anaungwa mkono kwa asilimia 100 na wamiliki wa klabu hiyo licha ya mwenendo mbaya wa matokeo katika Premier League. Chelsea wamepoteza mechi nne mfululizo, ikiwa ni pamoja na kichapo cha mabao 1-0 nyumbani dhidi ya Manchester United mwishoni mwa wiki.
Matokeo hayo yamewaacha Chelsea katika nafasi ya sita wakiwa na pointi 48 huku zikiwa zimesalia mechi tano, na matumaini yao ya kufuzu UEFA Champions League yakianza kufifia. Tatizo kubwa limekuwa ukosefu wa mabao, kwani timu hiyo haijafunga katika mechi zake nne za mwisho za ligi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza na waandishi wa habari, Rosenior alisema, “Nina uhakika wa asilimia 100 kuwa wamiliki bado wana imani nami. Mazungumzo yetu ya kila siku yamekuwa ya kunitia moyo na kunipa sapoti.”
Aliongeza kwa kusema, “Tunajua tunahitaji kushinda sasa, lakini hilo halipingani na malengo yetu ya mafanikio ya muda mrefu. Hata hivyo, hatujafanya vizuri katika mechi za karibuni na hilo ni jukumu langu kama kocha mkuu.
Kuhusu hali ya kikosi, Rosenior alibainisha kuwa mchezaji Estevao hatakuwepo katika mchezo ujao dhidi ya Brighton & Hove Albion, huku Joao Pedro akitarajiwa kufanyiwa tathmini ya mwisho kabla ya uamuzi wa kucheza.

