Kocha wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa, amejitokeza hadharani kumtetea mshambuliaji nyota Kylian Mbappe kufuatia lawama zilizomkumba baada ya kichapo cha UEFA Champions League dhidi ya Bayern Munich.
Real Madrid waliondoshwa kwenye mashindano hayo baada ya kupoteza kwa jumla ya mabao 6-4, huku wakichapwa 4-3 katika mchezo wa marudiano uliokuwa na ushindani mkubwa. Hali ilizidi kuwa ngumu baada ya Eduardo Camavinga kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 86, jambo lililoruhusu Bayern kufunga mabao mawili ya haraka na kuzua mjadala kuhusu mchango wa Mbappe katika ulinzi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya mchezo dhidi ya Deportivo Alaves, Arbeloa alisema, “Sina cha kumlaumu Kylian. Alikuwa katika kiwango cha juu, alifunga katika mechi zote mbili na alikuwa tishio muda wote kwa wapinzani.”
Aliendelea kusisitiza mchango wa mchezaji huyo akisema, “Alijituma hata katika majukumu ya ulinzi na alifanya kazi kubwa sana. Nimeridhishwa kabisa na kiwango chake katika mechi hiyo.”
Licha ya Mbappe kufunga mabao 40 katika mashindano yote msimu huu, atalazimika kusubiri tena kutimiza ndoto yake ya kutwaa taji la UEFA Champions League. Wakati huo huo, hatma ya Arbeloa ndani ya klabu hiyo bado haijawa wazi, huku Barcelona wakiwa mbele kwa pointi tisa katika mbio za ubingwa wa La Liga.

