Mbeya City Yamtimua Kocha Maxime Baada ya Kipigo cha 6-0 Dhidi ya Yanga

Klabu ya Mbeya City FC imetangaza rasmi kusitisha mkataba na kocha wake mkuu, Mecky Maxime, pamoja na benchi lake la ufundi, kufuatia makubaliano ya pande zote mbili.

Mbeya City Yamtimua Kocha Maxime Baada ya Kipigo cha 6-0 Dhidi ya YangaUamuzi huo umetolewa kupitia taarifa rasmi ya klabu hiyo kwa umma, ukieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuleta mabadiliko ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya Mbeya City kupokea kipigo    kizito cha mabao 6-0 kutoka kwa mabingwa watetezi Yanga. Matokeo hayo yameonekana kuwa kichocheo kikubwa cha mabadiliko hayo.

Mbeya City Yamtimua Kocha Maxime Baada ya Kipigo cha 6-0 Dhidi ya YangaKatika taarifa yake, uongozi wa klabu ulieleza kuwa, “Tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Kocha Mecky Maxime pamoja na wasaidizi wake. Tunatambua na kuthamini jitihada walizozifanya katika kipindi chote walichokuwa nasi.” Kauli hiyo inaonesha kuwa licha ya matokeo mabaya ya hivi karibuni, mchango wa benchi la ufundi umetambuliwa.

Mbeya City Yamtimua Kocha Maxime Baada ya Kipigo cha 6-0 Dhidi ya YangaAidha, klabu hiyo iliongeza kwa kusema, “Tunamshukuru Kocha Maxime kwa mchango wake na tunamtakia kila la kheri katika hatua zake zijazo.” Wasaidizi walioguswa na uamuzi huo ni pamoja na kocha msaidizi Nizar Khalfa na kocha wa viungo Francis Mkanula, ambao nao wameondoka sambamba na kocha mkuu.Kwa sasa, Mbeya City FC inatarajiwa kuanza mchakato wa kutafuta kocha mpya atakayechukua nafasi hiyo, huku lengo likiwa ni kurejesha ushindani ndani ya ligi kuu ya NBC.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.