Kasarani, Moi Kufungwa Kwa ajili ya Ukarabati Mkubwa Kuelekea AFCON 2027

Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi, Kasarani, unatarajiwa kufungwa rasmi ili kupisha matengenezo makubwa kuelekea michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027. Hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi ya kuhakikisha Kenya inakuwa tayari kushiriki kikamilifu katika mashindano hayo ya kihistoria.

Kasarani, Moi Kufungwa Kwa ajili ya Ukarabati Mkubwa Kuelekea AFCON 2027Kwa mujibu wa taarifa za ukaguzi wa serikali ulioshirikisha washauri, wakandarasi pamoja na wataalamu wa kiufundi kutoka Sports Kenya, ukarabati huo unalenga kuufikisha uwanja huo katika viwango vya kimataifa vinavyotakiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). “Lazima tuhakikishe miundombinu yetu inakidhi viwango vya juu kabisa kabla ya mashindano kuanza,” imeelezwa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

AFCON 2027 inatarajiwa kuwa ya kipekee kwa kuwa itafanyika kwa mara ya kwanza katika nchi tatu za Afrika Mashariki Tanzania, Kenya na Uganda chini ya mpango wa pamoja unaojulikana kama “Pamoja Bid”. Mashindano hayo yamepangwa kuanza Juni 19, 2027 na kumalizika Julai 18, 2027.

Kasarani, Moi Kufungwa Kwa ajili ya Ukarabati Mkubwa Kuelekea AFCON 2027

Kwa upande wa Tanzania, viwanja vitakavyotumika ni pamoja na Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam unaoendelea kufanyiwa ukarabati, Samia Suluhu Hassan Stadium jijini Arusha unaojengwa upya, pamoja na Amaan Stadium Zanzibar ambao tayari umeboreshwa kwa kiwango kikubwa.

Kasarani, Moi Kufungwa Kwa ajili ya Ukarabati Mkubwa Kuelekea AFCON 2027Nchini Kenya, pamoja na Kasarani, viwanja vingine ni Talanta Sports City (Nairobi) kinachojengwa upya, Nyayo National Stadium kinachofanyiwa ukarabati, pamoja na Kipchoge Keino Stadium kilichopo Eldoret kinachoboreshwa. “Hii ni fursa ya kuonyesha uwezo wa Kenya katika kuandaa mashindano makubwa,” imebainishwa.

Kasarani, Moi Kufungwa Kwa ajili ya Ukarabati Mkubwa Kuelekea AFCON 2027Kwa upande wa Uganda, maandalizi yanaendelea kupitia Mandela National Stadium (Namboole) ambayo tayari imekarabatiwa, pamoja na viwanja vipya vya Hoima City Stadium na Akii Bua Stadium. Kwa ujumla, maandalizi haya yanaashiria dhamira ya nchi za Afrika Mashariki kuhakikisha AFCON 2027 inakuwa ya mafanikio makubwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.