Ligi kuu ya NBC Tanzania inatarajiwa kuendelea leo hii kwa michezo miwili ambapo mchezo wa mapema kabisa ni huu wa Fountain Gate dhidi ya Simba.

Mchezo huo utapigwa majira ya saa 10:00 jioni katika dimba la Sheikh Amri Abeid Karume huku ushindi ukiwa ni muhimu sana kwa timu zote mbili.
Simba wametoka kutoa suluhu kwenye mechi yao iliyopita na kuangusha pointi 2 huku Fountain Gate wao wametoka kupoteza ugenini kwa mabao mengi kabisa na kufanya wazidi kuwa kwenye hali mbaya kwenye msimamo wa ligi.
Mpaka sasa timu hiyo ipo kwenye nafasi ya 14 wakiwa na pointi 16 kwenye michezo 17 waliyocheza hadi sasa, yaani wanatakiwa kufanya kila wawezalo kwenye mechi zao ambazo zimesalia wapata matokeo chanya.


