Aliyekuwa kocha mkuu wa Inter Miami, Javier Mascherano, ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wake akitaja sababu binafsi, miezi michache tu baada ya kuiongoza timu hiyo kufikia mafanikio makubwa zaidi katika historia ya klabu.
Mascherano alithibitisha uamuzi huo kupitia taarifa rasmi, akieleza shukrani zake kwa uongozi wa klabu, benchi la ufundi pamoja na wachezaji kwa ushirikiano wao uliowezesha mafanikio hayo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Ningependa kutangaza kuwa, kwa sababu binafsi, nimeamua kumaliza muda wangu kama kocha mkuu wa Inter Miami. Kwanza kabisa, naishukuru klabu kwa kuniamini, wafanyakazi wote kwa juhudi zao, lakini zaidi wachezaji ambao walifanya nyakati zisizosahaulika ziwezekane,” alisema Mascherano.
Aidha, alitoa shukrani zake kwa mashabiki na familia ya klabu kwa mchango wao mkubwa katika safari hiyo ya mafanikio.
“Ninawashukuru pia mashabiki na familia ya klabu, kwa sababu bila wao haya yote yasingewezekana. Nitabaki na kumbukumbu ya kombe letu la kwanza moyoni mwangu, na popote nitakapokwenda nitaendelea kuwatakia kila la heri,” aliongeza.
Kwa upande wake, mmiliki mwenza wa klabu hiyo, Jorge Mas, alisifu mchango wa Mascherano akisema kuwa ataendelea kuwa sehemu ya historia ya Inter Miami kutokana na mafanikio na mfano wa kujituma aliouonyesha.
“Javier atabaki kuwa sehemu ya historia ya klabu hii. Sio tu kwa makombe tuliyoshinda kama MLS Cup au mafanikio yetu katika Kombe la Dunia la Klabu, bali pia kwa mfano aliouweka kila siku kupitia bidii na kujitolea kwake. Tunaheshimu uamuzi wake na tunamshukuru kwa kila kitu,” alisema Jorge Mas.
Katika msimu wa 2025 ambao ulikuwa wa kwanza kwake kuinoa timu hiyo, Mascherano aliandika historia kwa kuipa klabu makombe mawili makubwa, likiwemo taji la kwanza la MLS Cup, huku pia timu ikivunja rekodi kwa kufunga mabao 101 ndani ya msimu mmoja.
Wakati huo huo, Inter Miami imetangaza kuwa Guillermo Hoyos atachukua nafasi ya ukocha mkuu, huku Alberto Marrero akiteuliwa kuwa mkurugenzi wa michezo kwa kipindi kijacho.

