Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, hatimaye amefungua akaunti ya mabao akiwa na Le Havre AC baada ya kufunga katika sare ya 1-1 dhidi ya wapinzani wao kwenye mchezo wa Ligue 1 uliochezwa Jumapili, Aprili 12, 2026.
Mchezo huo ulipigwa katika Uwanja wa Allianz Riviera, ambapo Samatta aliipatia timu yake bao la kuongoza dakika ya 41 kwa kumalizia pasi safi kutoka kwa Rassoul Ndiaye.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Bao hilo linakuwa la kwanza kwa mshambuliaji huyo tangu ajiunge na Le Havre katika dirisha kubwa la usajili la majira ya kiangazi, baada ya kukaa muda bila kufunga tangu aanze kuitumikia klabu hiyo ya Ufaransa.
Katika mchezo huo, Samatta alionyesha kiwango kizuri kabla ya kutolewa nje dakika ya 87 na nafasi yake kuchukuliwa na Stephan Zagadou, huku timu hizo zikigawana pointi mojamoja.
Mafanikio hayo yanaendelea kuonyesha mchango wa Samatta katika soka la kimataifa, hasa akiwa nahodha wa Taifa Stars na mchezaji tegemeo katika kikosi chake cha sasa.
Kwa bao hilo, Samatta ameweka rekodi ya kipekee kwa kufunga katika ligi tano tofauti barani Ulaya, hatua inayodhihirisha uzoefu na ubora wake katika soka la ushindani wa juu.

