Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imeingia rasmi kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa FIFA Series dhidi ya timu ya taifa ya Morocco utakaochezwa nchini Morocco.
Kikosi hicho tayari kimesafiri kuelekea Morocco kwa ajili ya maandalizi ya mwisho, huku benchi la ufundi likitazamia kutumia mchezo huo kama kipimo muhimu cha kiwango cha wachezaji dhidi ya moja ya timu bora barani Afrika.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Taarifa kutoka ndani ya kambi hiyo zinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa baadhi ya wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi kukosekana katika kikosi hicho kutokana na changamoto za upatikanaji wao katika dirisha hili la kimataifa.
Katika kikosi hicho, zaidi ya wachezaji 15 wametoka kwenye klabu ya JKT Queens, hali inayoifanya timu hiyo kuwa na uwakilishi mkubwa ndani ya Twiga Stars katika maandalizi haya.
Chanzo kutoka ndani ya timu kimeeleza sababu za kukosekana kwa baadhi ya wachezaji wa nje.
“Wachezaji wengi wanaocheza nje watakosa mechi hii kutokana na majukumu ya timu zao, na pia wametoka muda mfupi uliopita kwenye maandalizi ya WAFCON,” kilisema chanzo hicho.
Aidha, chanzo hicho kilisisitiza kuwa mechi hiyo ni fursa muhimu kwa benchi la ufundi kufanya tathmini ya kikosi.
“Kwa kuwa ni mechi ya kuangalia uwezo wa wachezaji, wale watakaopatikana kutoka nje na hawa wa ndani watachanganywa ili kuona namna bora ya kuboresha timu,” kiliongeza.

