Ibrahima Konaté Afunguka, Liverpool Kunyimwa Penalti Dhidi ya PSG

Beki wa Liverpool FC, Ibrahima Konaté, amesema kuwa uamuzi wa kutokutoa penalti kwa timu yake ulikuwa tukio la kuamua matokeo katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya waliopoteza dhidi ya Paris Saint-Germain.

Ibrahima Konaté Afunguka, Liverpool Kunyimwa Penalti Dhidi ya PSGTukio hilo lilitokea kipindi cha pili katika mchezo wa marudiano wa robo fainali uliopigwa Anfield, ambapo Alexis Mac Allister alianguka chini ya presha kutoka kwa Willian Pacho, na mwamuzi awali alitoa penalti kabla ya VAR kuingilia kati na kubatilisha uamuzi huo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Konaté alisema kuwa iwapo Liverpool wangepewa penalti hiyo na kufunga, mchezo ungeweza kubadilika kabisa huku matokeo yakiwa tofauti.

Ibrahima Konaté Afunguka, Liverpool Kunyimwa Penalti Dhidi ya PSG“Msimu uliopita tulipata penalti kama hiyo. Kwangu mimi ilikuwa penalti ya wazi kabisa, na alikuwa nyuma ya mwamuzi lakini hakupuliza filimbi, na inabidi tukubaliane na hilo,” alisema Konaté.

Liverpool FC walishindwa kurejea kwenye mchezo huo baada ya tukio hilo, huku Ousmane Dembélé akifunga mabao mawili yaliyoihakikishia Paris Saint-Germain ushindi wa jumla wa 4-0 na kutinga nusu fainali.

Konaté alieleza kuwa licha ya Liverpool kuonyesha kiwango kizuri, walikosa umakini katika kutumia nafasi walizopata. “Tulitengeneza nafasi nyingi na nadhani tulikuwa timu bora zaidi. Ilikuwa kidogo isiyo ya haki, kama msimu uliopita,” alisema.

Ibrahima Konaté Afunguka, Liverpool Kunyimwa Penalti Dhidi ya PSGAidha, aliitaka timu yake kujitahidi kurekebisha hali yao kwenye Ligi Kuu England, ambapo wanapambana kuhakikisha wanamaliza ndani ya nafasi tano za juu ili kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. “Ni kiwango cha chini kabisa kwa Liverpool kucheza Ligi ya Mabingwa. Tuna mechi sita zilizobaki na lazima tutoe kila kitu,” alisisitiza.

Konaté pia alituma salamu za pole kwa mshambuliaji Hugo Ekitike aliyeumia katika mchezo huo, akieleza wasiwasi wake kutokana na hali hiyo. “Nimepoteza maneno ya kusema kuhusu hilo. Naomba afueni, ni wakati mgumu sana kwake hasa kwa kuwa Kombe la Dunia linakuja,” alisema Konaté.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.