Collymore Amkosoa Salah, Asema Hakuaga Vizuri Liverpool

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Stan Collymore, ameonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa nyota wa klabu hiyo, Mohamed Salah, katika msimu wake wa mwisho akiwa Anfield. Collymore anaamini kuwa licha ya mchango mkubwa wa Salah, angeweza kushughulikia hali ya kuondoka kwake kwa namna bora zaidi.

Collymore Amkosoa Salah, Asema Hakuaga Vizuri Liverpool“Inasikitisha, lakini nadhani angeweza kulishughulikia hili kwa njia bora zaidi,” amesema Collymore.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Collymore alilinganisha namna ya kuaga ya Salah na ile ya Andy Robertson, akisema beki huyo alionesha heshima na shukrani kwa klabu kwa uwazi zaidi. Kwa upande wake, anaona Salah hakufikisha ujumbe huo kwa kiwango kilichotarajiwa.

“Ukiangalia video ya Robertson, alisema wazi kuwa anaondoka kwa shukrani baada ya miaka tisa ya mafanikio. Kwa Salah, ilikuwa tofauti kidogo,” aliongeza.

Collymore Amkosoa Salah, Asema Hakuaga Vizuri LiverpoolHata hivyo, Collymore alikiri kuwa tofauti ya nafasi zao uwanjani inaweza kueleza tabia hizo, akieleza kuwa washambuliaji mara nyingi huwa na kujiamini kwa kiwango kikubwa na huchukulia mambo binafsi wanapopoteza nafasi au kupungua kiwango.

“Washambuliaji ni tofauti na mabeki, wana imani kubwa sana na uwezo wao, hivyo wakiachwa benchi wanachukulia kwa uzito zaidi,” alisema.

Collymore Amkosoa Salah, Asema Hakuaga Vizuri LiverpoolLicha ya hayo, Collymore alisisitiza kuwa mafanikio ya Salah Liverpool hayawezi kutenganishwa na mchango wa klabu hiyo kwake, akibainisha kuwa pande zote mbili zilifaidika kwa kiasi kikubwa. “Watu wanasema Salah amekuwa mzuri sana kwa Liverpool, lakini pia Liverpool imekuwa nzuri sana kwa Salah,” alisisitiza.

Collymore Amkosoa Salah, Asema Hakuaga Vizuri LiverpoolAkizungumzia mustakabali wa klabu hiyo, Collymore anaamini Liverpool itaendelea mbele bila matatizo na hatimaye itapata mchezaji mwingine wa kuchukua nafasi ya Salah, akisisitiza kuwa hakuna mchezaji aliye mkubwa kuliko klabu. “Liverpool itaendelea na itampata mchezaji mwingine atakayechukua nafasi yake, hakuna mchezaji aliye mkubwa kuliko klabu,” alihitimisha.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.