Kocha mpya wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi, amesema kuwa wachezaji wake wanahitaji msaada wa karibu zaidi wa kisaikolojia kama wa “baba” badala ya maelekezo ya kawaida ya ukocha, kufuatia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Sunderland AFC.
De Zerbi alichukua mikoba ya ukocha mwishoni mwa mwezi uliopita akichukua nafasi ya kocha wa muda Igor Tudor, lakini alianza vibaya baada ya Spurs kupoteza mchezo huo uliowaacha katika hatari ya kushuka daraja kwenye Premier League.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Bao pekee la mchezo lilifungwa kipindi cha pili na Nordi Mukiele, likiwa limepata mguso uliobadili mwelekeo, na kuifanya Tottenham kubaki nyuma kwa pointi mbili dhidi ya West Ham United huku zikiwa zimesalia mechi sita pekee msimu huu.
Spurs hawajapata ushindi wowote wa ligi tangu Desemba mwaka jana, na sasa wanakabiliwa na hatari ya kushuka daraja kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1977, jambo linaloonyesha ukubwa wa changamoto aliyonayo De Zerbi.
Akizungumza baada ya mchezo huo, De Zerbi alisisitiza kuwa ushindi mmoja unaweza kubadilisha hali ya timu hiyo.
“Tunapaswa kupigania ushindi mmoja kwa sababu ushindi mmoja unaweza kubadilisha kila kitu msimu huu,” alisema.
Kocha huyo alikiri kuwa timu yake ina ubora lakini inakosa kujiamini, akisisitiza umuhimu wa mshikamano na kujiamini zaidi.
“Wachezaji wana ubora mkubwa, lakini tunapaswa kujiamini zaidi. Jambo muhimu zaidi sasa ni kushinda mechi moja,” aliongeza.
De Zerbi pia alieleza kuwa changamoto kubwa si uwezo wa soka bali ni hali ya kisaikolojia ya wachezaji wake.
“Naweza kuwa kama kaka au baba kwao, hawahitaji kocha kwa sasa. Hawahitaji kuboresha soka lao, watafanya vizuri zaidi tutakapopata kujiamini,” alihitimisha.

