Kocha wa Chelsea FC, Liam Rosenior, amesema timu hiyo ipo katika “wakati mgumu” kufuatia kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Manchester City kilichochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
Katika mchezo huo, mabao ya Nico O’Reilly, Marc Guehi na Jeremy Doku yalifungwa kipindi cha pili, yakiongeza presha kwa Rosenior ambaye timu yake inaendelea kusuasua katika mbio za kumaliza nafasi za juu kwenye Premier League.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Chelsea kwa sasa ipo nafasi ya sita, ikiwa nyuma kwa pointi nne dhidi ya Liverpool FC wanaoshika nafasi ya tano, huku matumaini yao ya kufuzu UEFA Champions League yakizidi kufifia.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Rosenior alikiri kiwango cha timu yake hasa kipindi cha pili hakikuwa cha kuridhisha.
“Hatukuwa vizuri kabisa kipindi cha pili. Ni hadithi ile ile ya mwezi mzima sasa, hasa namna tunavyokabiliana na changamoto tunapopoteza,” alisema.
Kocha huyo alisisitiza umuhimu wa timu kubaki imara wanapopoteza mabao dhidi ya wapinzani wakubwa.
“Unapocheza dhidi ya timu bora kama hii na ukafungwa, unapaswa kubaki kwenye mchezo kwa dakika chache zinazofuata. Lakini kipindi cha pili kilikuwa kigumu sana kwetu,” aliongeza.
Mashabiki wa Chelsea waliizomea timu yao baada ya mchezo kumalizika, huku Rosenior akichukua lawama na kuahidi maboresho.
“Ninawajibika. Hili ni kundi na tunapaswa kuboresha. Sidhani kama kulikuwa na ukosefu wa juhudi, lakini kulikuwa na ukosefu wa kujiamini kipindi cha pili,” alisema.
Chelsea imepoteza michezo mitano kati ya sita iliyopita katika mashindano yote, ikiwa ni pamoja na kupoteza mechi tatu mfululizo za ligi bila kufunga bao lolote. Hali hiyo imezidi kuongeza presha kuelekea michezo iliyosalia msimu huu.
Wakati huohuo, kiungo Enzo Fernandez alikosekana kwa mechi ya pili mfululizo baada ya kusimamishwa na kocha wake kufuatia kauli zake kuhusu uwezekano wa kuondoka klabuni hapo majira ya joto. Hata hivyo, Rosenior amethibitisha kuwa mchezaji huyo atarejea kikosini wiki ijayo.
“Hakuna timu ambayo haitamhitaji Enzo. Tulifanya uamuzi huu kwa manufaa ya muda mrefu ya klabu. Amezungumza na mimi na wachezaji wenzake, na atarejea kikosini Jumanne. Ni mchezaji mkubwa na mtu mzuri,” alihitimisha Rosenior.

