Mshambuliaji wa Aston Villa, Ollie Watkins, amesema bado ana matumaini ya kurejea katika kikosi cha timu ya taifa ya uingereza kwa ajili ya Kombe la Dunia, licha ya kukosekana kwenye kikosi cha mechi za kirafiki mwezi uliopita dhidi ya Uruguay na Japan.
Watkins anaamini kuwa nafasi yake bado ipo wazi endapo ataendelea kufanya vizuri katika michezo iliyosalia ya msimu. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye tayari ameichezea England mara 20 na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshiriki UEFA Euro 2024, aliachwa nje ya kikosi cha wachezaji 35 kilichotajwa na kocha Thomas Tuchel. Uamuzi huo ulitokana na kushuka kwa kiwango chake cha ufungaji kwa muda mrefu katika msimu huu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hata hivyo, tangu kutotajwa kwake, Watkins ameonekana kurejea katika kiwango chake bora baada ya kufunga mabao manne katika michezo minne mfululizo. Akiwa na Aston Villa, alifanikiwa pia kufunga bao lake la 100 katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bologna kwenye michuano ya UEFA Europa League.

Akizungumza na moja ya Chombo cha habari Watkins alisema, “Ninachoweza kufanya ni kuendelea kufunga mabao. Nilivunjika moyo kutokuwepo kwenye kikosi kilichopita, lakini ninaelewa sababu za kocha kutonichagua.” Kauli hiyo inaonesha dhamira yake ya kupambana kurejea katika kikosi cha taifa.
Aliongeza kwa kusema, “Lazima niruhusu uwanjani ndio paongee kwa niaba yangu. Nitaendelea kufanya vizuri na kufunga mabao mengi iwezekanavyo hadi mwisho wa msimu.” Maneno hayo yanaakisi azma yake ya kurejesha imani kwa benchi la ufundi la England.
Wakati huo huo, England inajiandaa kwa michezo ya kirafiki dhidi ya New Zealand na Costa Rica mwezi Juni kama sehemu ya maandalizi ya Kombe la Dunia litakalofanyika katika nchi za Marekani, Canada na Mexico kuanzia Juni 11 hadi Julai 19. England itaanza kampeni yake ya Kundi L kwa kuikabili Croatia kabla ya kucheza na Ghana na Panama katika ratiba ya mashindano hayo.

