Kocha wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema maandalizi ya timu yake kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania yameenda vizuri, huku akisisitiza kuwa wanatarajia upinzani mkali kutokana na ubora wa wapinzani wao msimu huu.
Ibenge amesema kuwa mchezo huo ni miongoni mwa mechi anazozipenda kuongoza kutokana na ushindani wake mkubwa, jambo linalowapa wachezaji motisha ya kuongeza bidii na kuhakikisha wanapata matokeo chanya uwanjani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Tunaiheshimu JKT Tanzania kwa sababu ni timu ngumu na inayopambana sana. Maandalizi yetu yamekuwa mazuri na tuko tayari kwa mchezo,” alisema Ibenge.
Kwa upande wake, kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Nassor Saadun, amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri na wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo muhimu wa ligi.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex, kuanzia saa 1:00 usiku, ukiwa ni sehemu ya msimu wa Ligi Kuu ya NBC nchini Tanzania.

