Real Madrid Yaanza Mikakati Yakumpata Kocha Mpya Baada ya Kutolewa UCL

Klabu ya Real Madrid imeanza mchakato wa kusaka kocha mpya baada ya kutolewa katika michuano ya UEFA Champions League kufuatia kipigo cha mabao 4-3 (jumla 6-4) dhidi ya Bayern Munich katika mchezo uliopigwa mjini Munich.

Real Madrid Yaanza Mikakati Yakumpata Kocha Mpya Baada ya Kutolewa UCLUongozi wa klabu hiyo chini ya rais Florentino Pérez umeanza kuangalia machaguo mbalimbali ya makocha watakaochukua nafasi hiyo msimu ujao, huku lengo likiwa ni kurejesha ubora wa timu katika mashindano ya Ulaya.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Miongoni mwa majina yanayoripotiwa kuingia kwenye orodha hiyo ni Jürgen Klopp, ambaye anatajwa kuwa kipaumbele cha juu, ingawa bado hakuna mawasiliano rasmi yaliyofanyika kati yake na klabu hiyo ya Hispania.

Real Madrid Yaanza Mikakati Yakumpata Kocha Mpya Baada ya Kutolewa UCLPia kocha Mauricio Pochettino anatajwa kuwa mgombea mwenye nafasi kubwa zaidi kutokana na urahisi wa kupatikana kwake, huku Zinedine Zidane na Didier Deschamps nao wakiwekwa kwenye orodha ya mbadala wanaofikiriwa.

Real Madrid Yaanza Mikakati Yakumpata Kocha Mpya Baada ya Kutolewa UCLKushindwa kwa kocha Álvaro Arbeloa kuifikisha timu hiyo hatua ya juu zaidi katika mashindano ya Ulaya kumechochea uongozi wa Real Madrid kuanza upya mipango ya benchi la ufundi, huku mustakabali wake ukiwa bado haujathibitishwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.