Mshambuliaji wa Bayern Harry Kane amempongeza Luis Diaz baada ya mchango wake mkubwa uliosaidia klabu hiyo kuiondoa Real Madrid na kutinga hatua ya nusu fainali ya UEFA Champions League.
Bayern ilikuwa na faida ya mabao 2-1 kutoka mchezo wa kwanza, lakini ilijikuta nyuma mara tatu katika kipindi cha kwanza kutokana na mchezo mkali wa Real Madrid. Hata hivyo, mchezo uligeuka dakika za mwisho baada ya Diaz kufunga bao la ushindi dakika ya 89, kabla ya Michael Olise kuongeza bao la nne katika muda wa nyongeza, na kuifanya Bayern ishinde 4-3 na jumla ya 6-4.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
alisema Kane. “Dakika za mwisho zilihisi kama sisi ndio tulikuwa timu inayotafuta suluhisho zaidi,” “Walianza kuchoka kidogo, na wakati mwingine unahitaji tu moment ya ubunifu, shuti la ajabu au pasi ya kipekee. Hapa Diaz na Olise walifanya kazi kubwa kumaliza mchezo.”
Kane pia alieleza kuwa subira ya kikosi chao ilichangia mafanikio hayo dhidi ya mabingwa hao wa kihistoria. “Mabadiliko ya hisia katika kipindi cha kwanza yalikuwa ya kipekee, lakini tulibaki kwenye mchezo na tulikuwa na subira. Tulijua kadri muda unavyokwenda tutazidi kuwa bora,” aliongeza.
Bao alilofunga Kane pia limemfanya kuwa mchezaji wa kwanza Mwingereza katika ligi tano bora Ulaya kufikisha mabao 50 katika mashindano yote ndani ya msimu mmoja. “Ni matokeo ya kazi kubwa ya timu nzima, sio mimi peke yangu. Nitaendelea kujituma,” alisema.
Kocha wa Bayern, Vincent Kompany, alisema timu yake iko tayari kwa changamoto ya nusu fainali dhidi ya PSG. “Tunaamini zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Tulipambana hadi mwisho bila kukata tamaa dhidi ya Real Madrid, na sasa tuko tayari kwa hatua inayofuata,” alisema Kompany.

