Klabu ya Azam FC ipo tayari kuivaa Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa Aprili 2 kwenye Dimba la Airtel, mkoani Singida, huku lengo likiwa kuendeleza ushindani wao kwenye msimamo wa ligi.
Baada ya mchezo huo mgumu, Azam FC wanatarajiwa kurejea Dar es Salaam kujiandaa na pambano lingine zito dhidi ya Simba SC ambao watakuwa wageni kwenye mchezo huo, hali inayoongeza uzito wa ratiba yao ya mechi zijazo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Wakati huo huo, nyota kadhaa wa Azam FC akiwemo Feisal Salum, Aishi Manula, pamoja na Foba, Nado, Twalib na Lameck Lawi, wanatarajiwa kurejea nchini baada ya kuitumikia Taifa Stars katika mechi za kimataifa za FIFA series nchini Rwanda.
Kwa mujibu wa taarifa, wachezaji hao wanatarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kuelekea moja kwa moja mkoani Singida kuungana na wenzao kambini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.

