Manchester United wamepewa ujumbe mzito kuwa jaribio lolote la kumsajili Cole Palmer litahitaji dau la hali ya juu la pauni milioni 200. Kiungo huyo mshambuliaji wa Chelsea ameendelea kuwa mhimili mkuu wa kikosi, huku thamani yake sokoni ikiendelea kupanda licha ya kusumbuliwa na majeraha msimu huu.

Tangu ajiunge na Chelsea mwaka 2023 akitokea Manchester City, Palmer amekuwa mchezaji muhimu sana, akichangia mabao 53 na asisti 32 katika mechi 122. Hata hivyo, msimu huu amekumbwa na changamoto za kiafya, ikiwemo tatizo la nyonga na jeraha la kidole cha mguu, jambo lililopunguza makali yake hadi mchango wa mabao 13 pekee.
Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Scott Sinclair, anaamini Palmer bado ni miongoni mwa wachezaji bora kabisa katika Ligi Kuu England. Amesisitiza kuwa uwezo wake wa kubadilisha mchezo kwa muda mfupi ndio unaomfanya kuwa na thamani kubwa kiasi hicho.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hata hivyo, Sinclair ameweka wazi kuwa hatma ya Palmer inaweza kuathiriwa na mafanikio ya Chelsea katika kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kukosekana kwenye michuano hiyo kunaweza kumfanya mchezaji huyo kufikiria upya mustakabali wake.

Kwa sasa, Palmer ana mkataba wa muda mrefu hadi mwaka 2033, jambo linaloipa Chelsea nguvu kubwa katika mazungumzo yoyote ya usajili. Hivyo, klabu yoyote itakayohitaji huduma yake italazimika kuvunja rekodi ili kuweza kumng’oa Stamford Bridge.

