Jose Mourinho ameweka wazi msimamo wake kuhusu mustakabali wake ndani ya Benfica, akisisitiza kuwa ataendelea kubaki klabuni hapo bila kujali kiwango cha uwekezaji kitakachofanywa kwenye usajili msimu ujao. Baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Nacional, kocha huyo ameonyesha kuwa tayari anawaza zaidi kuhusu msimu ujao.

Licha ya Benfica kubaki nyuma kwa pointi saba dhidi ya vinara FC Porto, Mourinho anaonekana kutulia na mkakati wake wa muda mrefu. Ameweka wazi kuwa hategemei usajili mkubwa ili kubaki, bali anaamini katika kujenga timu imara kupitia rasilimali zilizopo ndani ya klabu.
Kocha huyo maarufu amesema wazi kuwa mustakabali wake uko mikononi mwake mwenyewe, na hana masharti yoyote kwa uongozi. Kauli yake inaonyesha uaminifu mkubwa kwa mradi wake na dhamira ya kuurudisha ubora wa Benfica kwa njia ya kimkakati badala ya matumizi makubwa ya fedha.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Sehemu muhimu ya mpango wake ni kukuza vipaji kutoka akademi ya Seixal, ambayo imekuwa ikizalisha wachezaji bora kwa miaka mingi. Mourinho anataka kutumia kipindi cha maandalizi ya msimu, hasa wakati wa majukumu ya timu za taifa, kuwapa nafasi vijana wenye vipaji kuingia kikosi cha kwanza.

Hata hivyo, kabla ya kufika huko, Benfica wana kibarua kizito mbele yao katika derby dhidi ya Sporting CP. Hii ni mechi muhimu ambayo inaweza kuamua hatima ya mbio za ubingwa, huku Mourinho akihitaji ushindi ili kuendeleza matumaini yao.


