Tottenham Wako Kwenye Hatihati Kubaki Ama Kushuka Daraja

Tottenham Hotspur wako kwenye vita ya kusalia Ligi Kuu, na makamu nahodha Micky van de Ven ameweka wazi kwamba muda wa kujifunza mfumo mpya wa Roberto De Zerbi unaisha haraka. Baada ya kipigo cha 1-0 dhidi ya Sunderland, Spurs wamezama kwenye hatari, huku mechi sita tu zikisalia kuamua hatima yao.

Tottenham Wako Kwenye Hatihati Kubaki Ama Kushuka Daraja

De Zerbi aliingia na falsafa ya soka la kuvutia, kuanzia build-up kutoka nyuma hadi kumiliki mpira. Lakini uhalisia wa uwanja ni mkali zaidi kuliko vitabu vya mbinu. Tottenham wanahitaji matokeo sasa. Van de Ven anasisitiza wazi kwama mfumo ni muhimu, lakini pointi ndizo zinazoamua kama unabaki au unashuka daraja.

Presha imekuwa nzito huku Tottenham wakiwa hawajashinda hata mechi moja tangu mwaka 2026 uanze, rekodi mbaya inayowaweka karibu na kushuka daraja. Timu kama Derby (2008), Sunderland (2003), na Swindon (1993) waliwahi kupitia mwanzo mbaya zaidi na wote waliishia kushuka.

Tottenham Wako Kwenye Hatihati Kubaki Ama Kushuka Daraja

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza kwa hisia kali, Van de Ven alikiri kuwa timu haichezi vibaya kabisa, lakini bahati haipo upande wao. Nafasi zinatengenezwa, lakini hazizai mabao. Na kila filimbi ya mwisho inapolia bila ushindi, mzigo wa kisaikolojia unaongezeka. Kujiamini kumeporomoka, na sasa wanahitaji kuurudisha haraka kama wanataka kuishi kwenye ligi.

Tottenham Wako Kwenye Hatihati Kubaki Ama Kushuka Daraja

Sasa kila mechi ni kama fainali. Brighton na Wolves wanawasubiri mwezi huu, kabla ya Mei yenye vita kali dhidi ya Aston Villa, Leeds, Chelsea na Everton siku ya mwisho. Hapa hakuna nafasi ya makosa, Tottenham wanapaswa kuunganisha haraka mfumo wa De Zerbi na kupata matokeo papo hapo. Vinginevyo, historia mbaya inaweza kuandikwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.