Carrick Asukuma Kwa Kasi Mpango Wa Usajili Wa Mainoo

Manchester United wako katika hatua za mwisho za kumpa Kobbie Mainoo mkataba mpya wa muda mrefu, huku kocha Michael Carrick akithibitisha kuwa mazungumzo yanaenda vizuri kabisa. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 ameonekana kuwa mhimili mpya wa timu, na klabu imedhamiria kumbakiza.

Carrick Asukuma Kwa Kasi Mpango Wa Usajili Wa Mainoo

Mainoo amepanda kiwango kwa kasi ndani ya mfumo mpya wa Carrick. Kutoka kuwa na nafasi chache chini ya Ruben Amorim, sasa amekuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza, akianza mechi zote za Ligi Kuu tangu mabadiliko ya benchi la ufundi. Na mshahara wake unatarajiwa kupanda kutoka takribani £25,000 hadi £120,000 kwa wiki.

Carrick ameweka wazi kuwa hana presha lakini ana imani kubwa na mazungumzo hayo. Akiwa na utulivu wa kocha anayejenga kitu kikubwa, alisema klabu iko mahali pazuri na hatua zinakaribia kukamilika. Kauli yake imeongeza morali kwa mashabiki ambao tayari wanaona Mainoo kama injini ya kizazi kipya cha United.

Carrick Asukuma Kwa Kasi Mpango Wa Usajili Wa Mainoo

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

United wameshikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, wakiwa na faida ya alama saba dhidi ya Chelsea walioko nafasi ya sita, pamoja na mechi moja mkononi dhidi ya Leeds. Huu ni ushindani wa moto kwelikweli, hasa msimu huu ambao EPL inatoa nafasi tano za Champions League.

Carrick Asukuma Kwa Kasi Mpango Wa Usajili Wa Mainoo

Na sasa macho yote yanaelekezwa kwenye pambano lijalo dhidi ya Leeds. Katika mbio hizi za mwisho dhidi ya Chelsea, Liverpool, Brentford, Forest na Brighton, United wanahitaji kutokudondosha alama ovyo ili kuendelea kuishikiria nafasi ya tatu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.