Juventus Wamefikia Makubaliano ya Kumuongezea Mkataba Manuel Locatelli Hadi Mwaka 2030

Juventus wamemfunga rasmi Manuel Locatelli hadi mwaka 2030 kwa mshahara unaokadiriwa kuwa karibu €4m, akipongezwa kwa uongozi wake ndani ya timu.

Juventus Wamefikia Makubaliano ya Kumuongezea Mkataba Manuel Locatelli Hadi Mwaka 2030

Sassuolo wamethibitisha kuwa Juventus wanabaki na asilimia 50 ya mauzo ya baadaye ya Tarik Muharemovic, jambo linaloweza kuwanufaisha kifedha iwapo atauzwa baada ya kufanya vizuri Serie A na timu ya taifa ya Bosnia.

Juventus pia wanafuatilia nahodha wa Sporting CP Morten Hjulmand, huku akihusishwa na uwezekano wa kuhamia, ingawa kutakuwa na ushindani mkubwa.

Kuhusu Emil Holm, baada ya kuonyesha kiwango kizuri akitokea majeruhi, mustakabali wake utajadiliwa kati ya Juve na Bologna, ikiwa ni pamoja na kipengele cha €15m au mkopo mrefu zaidi kwa mchezaji huyo.

Juve mpaka sasa wapo nafasi ya 4 wakiwa na pointi zao 60 huku wakifukuzia nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya msimu huu kufanya vibaya.

Juventus Wamefikia Makubaliano ya Kumuongezea Mkataba Manuel Locatelli Hadi Mwaka 2030

Pia wikendi hii timu hiyo itashuka dimbani kusaka pointi 3 dhidi ya dhidi ya Bologna ambao nao walikuwa wakishiriki michuano ya Europa League ambayo wameondolewa baada ya kufungwa mechi zote mbili.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.