Mechi ya mkondo wa pili ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL kati ya Mamelodi Sundowns na Espérance de Tunis imethibitishwa kuwa SOLD OUT, na mashabiki wote tayari watajaa kuipa nguvu mechi hiyo kubwa.
Uwanja wa Loftus Versfeld unatarajiwa kufurika rangi ya njano na bluu, huku “Yellow Nation” ya Sundowns ikijivunia faida ya nyumbani katika mchezo huu muhimu wa kuamua mshindi wa tiketi ya fainali.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa upande mwingine, Espérance de Tunis wanaingia wakiwa na uzoefu mkubwa katika michuano ya Afrika, wakitegemea historia yao na ubora wa kikosi chao katika mechi za hatua za mtoano.
Mamelodi Sundowns wanabeba matumaini makubwa baada ya kupata ushindi katika mchezo wa kwanza, jambo linalowapa nafasi nzuri kuelekea mchezo huu wa marudiano.
Katika mchezo wa kwanza, Sundowns waliibuka na ushindi wa bao 1 lililofungwa na Brayan Muniz dakika za mapema kipindi cha pili, ingawa walilazimika kumaliza mechi wakiwa pungufu baada ya Grant Kekana kupewa kadi nyekundu dakika ya 84.
Sasa macho ya mashabiki wa soka barani Afrika yameelekezwa Loftus Versfeld, ambapo vita ya heshima kati ya soka la Afrika Kusini na Afrika Kaskazini itatoa majibu ya nani atasonga mbele fainali ya CAF Champions League.

