Klabu ya Al Ahly imetoa tamko rasmi kufuatia kuondolewa katika michuano ya CAF Champions League baada ya kufungwa jumla ya mabao 3-2 na ES Tunis, hatua iliyozua taharuki kwa mashabiki na wadau wa soka Nchini Misri na Afrika.
Kupitia kwa Rais wa klabu hiyo, Mahmoud El Khatib, uongozi umefanya kikao cha dharura na kukiri kuwepo kwa mapungufu ya kiufundi na kiutawala yaliyochangia matokeo hayo yasiyoridhisha katika mashindano hayo makubwa barani Afrika.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika hatua ya kurekebisha hali hiyo, klabu imesisitiza kuwa tayari imefikia maamuzi magumu yatakayohusisha mabadiliko mbalimbali, ambapo baadhi yatatangazwa hivi karibuni huku mengine yakisubiri kumalizika kwa msimu ili kulinda maslahi ya timu.
Aidha, uongozi umeeleza kuwa umeanza mchakato wa kufanya mageuzi makubwa ndani ya sekta ya soka ya klabu hiyo, yakilenga kurejesha ubora, utambulisho na hadhi ya Al Ahly kama moja ya klabu bora barani Afrika.
Ikumbukwe Al Ahly anashindwa kuingia fainali ya ligi ya mabingwa kwa mara ya pili mfululizo ambapo msimu jana bingwa alikuwa Pyramidi ya Nchini nmsri na mimu huu tayari ameshatolewa kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Katika hitimisho la tamko hilo, uongozi umeomba radhi mashabiki kwa huzuni na hasira waliyonayo kufuatia matokeo hayo, huku ukiahidi kuchukua hatua za haraka ili kurejesha mafanikio na imani ya wapenzi wa klabu hiyo

