Nguli wa soka England, Wayne Rooney, ameibuka na mshangao mkubwa kufuatia uamuzi wa kocha Thomas Tuchel kumuacha nje beki wa Real Madrid, Trent Alexander-Arnold, kwenye kikosi cha wachezaji 35 kwa ajili ya mechi za kirafiki. Uamuzi huo umeibua mjadala mkubwa, hasa ukizingatia ubora na uzoefu wa mchezaji huyo.

Rooney ameweka wazi kuwa ni ajabu kwa mchezaji wa kiwango cha Trent kukosekana kwenye kikosi kikubwa kama hicho. Ameeleza kuwa licha ya mapungufu yake ya ulinzi, uwezo wake akiwa na mpira ni wa kipekee na haupatikani kwa urahisi kwa wachezaji wengine wa England.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mbali na hoja za kiufundi, Rooney amezua mjadala mwingine kwa kudokeza uwezekano wa sababu za ndani ya kikosi. Amehoji kama kuna juhudi za kuvunja kundi maalum la wachezaji, akimtaja Jude Bellingham kama sehemu ya mjadala huo, kutokana na ukaribu wake na Trent.
Kauli hiyo imeongeza uzito wa mjadala kuhusu mazingira ya ndani ya timu ya taifa ya England, hasa katika kipindi hiki ambacho wanajiandaa kwa FIFA World Cup 2026. Imeibua maswali kuhusu maamuzi ya Tuchel na mwelekeo wa kikosi chake.

Kwa sasa, mustakabali wa Trent ndani ya timu ya taifa unaonekana kuwa na mashaka makubwa. Ikiwa ataendelea kukosa nafasi, huenda akaikosa michuano mikubwa ijayo, huku England wakilazimika kutafuta mbadala wa ubunifu wake mkubwa uwanjani.

