Vinicius JR Aibuka Shujaa, Real Madrid Ikiichapa Atletico 3-2

Nyota Vinicius Jr alifunga mabao mawili na kuiwezesha Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid katika dabi kali ya jiji la Madrid iliyochezwa dimba la Santiago Bernabéu.

Vinicius JR Aibuka Shujaa, Real Madrid Ikiichapa Atletico 3-2Ushindi huo ulikuwa wa kipekee kwa Vinicius Jr, ambaye alifanikiwa kuvunja ukame wake wa mabao dhidi ya Atletico katika La Liga baada ya kushindwa kufunga katika mechi 12 zilizopita dhidi ya wapinzani hao.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Real Madrid walianza mchezo kwa kasi, wakitengeneza nafasi kadhaa za mapema kupitia Dani Carvajal na Federico Valverde, huku Atletico nao wakijibu mashambulizi kupitia Marcos Llorente. Hata hivyo, Atletico ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia Ademola Lookman kabla ya mapumziko.

Vinicius JR Aibuka Shujaa, Real Madrid Ikiichapa Atletico 3-2Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Real Madrid, ambapo Vinicius Jr alisawazisha kwa mkwaju wa penalti kabla ya Valverde kuifungia timu yake bao la pili dakika chache baadaye. Atletico walirudi mchezoni kupitia bao kali la Nahuel Molina, lakini Vinicius Jr alijibu kwa bao la kuvutia lililohitimisha ushindi wa Real.

Kocha wa Atletico, Diego Simeone, alionekana kuwa na presha kubwa wakati wa mchezo huo, huku kocha wa Real Madrid Alvaro Arbeloa akiongoza dabi yake ya kwanza akiwa mtulivu zaidi. Mchezo huo pia ulimshuhudia Jude Bellingham akirejea uwanjani baada ya majeraha.

Vinicius JR Aibuka Shujaa, Real Madrid Ikiichapa Atletico 3-2Akizungumza baada ya ushindi huo, Vinicius Jr alisema “Ni ushindi muhimu sana kwetu, hasa dhidi ya wapinzani wetu wa karibu. Nilikuwa nasubiri muda mrefu kufunga dhidi yao na leo nimefanikiwa.”

Vinicius JR Aibuka Shujaa, Real Madrid Ikiichapa Atletico 3-2Kwa upande wake, Simeone alisema “Tulipambana hadi mwisho na tulikuwa karibu kupata matokeo. Ni mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa na maamuzi madogo yameamua matokeo.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.