Klabu ya Al Ahly SC imethibitisha kupokea barua rasmi kutoka kwa CAF ikieleza adhabu zilizotolewa na Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo kufuatia vurugu za mashabiki mwishoni mwa mchezo wa hatua ya makundi wa CAF Champions League.

Kupitia taarifa iliyotolewa katika majukwaa ya mitandao ya kijamii ya klabu hiyo, imeelezwa kuwa adhabu hizo zinajumuisha kuwapiga marufuku mashabiki wa Al Ahly kuhudhuria michezo miwili ijayo ya mashindano ya Afrika. Hata hivyo, klabu hiyo imefafanua kuwa adhabu ya mchezo wa pili imesimamishwa kwa muda.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika taarifa hiyo, klabu hiyo imesema imepokea barua kutoka CAF ikieleza uamuzi wa Kamati ya Nidhamu wa kuwazuia mashabiki wa Al Ahly kuhudhuria michezo miwili ijayo ya Afrika, huku adhabu ya mchezo wa pili ikiwa imesimamishwa. Hatua hiyo inamaanisha mchezo mmoja pekee ndio utachezwa bila mashabiki isipokuwa kama kutatokea kosa jingine.

Mbali na adhabu hiyo, CAF pia imeiwekea Al Ahly faini ya kifedha ya dola za Marekani 50,000 pamoja na adhabu ya ziada ya dola 10,000 kutokana na matumizi ya vifaa vya laser vilivyotumiwa na baadhi ya mashabiki wakati wa mchezo huo. Tukio hilo lilitokea katika mchezo kati ya Al Ahly SC na AS FAR uliochezwa katika Cairo International Stadium tarehe 15 Februari katika raundi ya mwisho ya hatua ya makundi. Ingawa mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana, baadhi ya mashabiki wa Al Ahly waliripotiwa kurusha chupa za maji kuelekea wachezaji wa AS FAR baada ya filimbi ya mwisho, tukio lililosababisha mchezo kusimama kwa muda kabla ya hali kurejea kuwa shwari.


