Aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Kenya Engin Firat, amefariki dunia baada ya kuripotiwa kupata mshtuko wa moyo katika uwanja wa Istanbul nchini Uturuki alipokuwa akisafiri kutoka Beirut kuelekea Adana.

Kocha huyo mwenye asili ya Uturuki na Ujerumani aliwahi kuinoa timu ya taifa ya Kenya kwa kipindi tofauti na kuacha alama katika maendeleo ya soka la taifa hilo kupitia mbinu na uzoefu wake mkubwa katika ukocha wa kimataifa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kabla ya kifo chake, Engin Firat alikuwa ametangazwa hivi karibuni kuwa kocha mpya wa klabu ya Al Nejmeh SC inayoshiriki ligi ya Lebanon, ambapo alitarajiwa kuanza majukumu yake mapya katika kipindi cha karibuni.

Kupitia taarifa rasmi, klabu ya Al Nejmeh SC imethibitisha kifo chake na kumkumbuka kama kocha aliyeacha mchango mkubwa katika soka la Kenya pamoja na wachezaji wengi aliowahi kufanya nao kazi katika taaluma yake ya ukocha.

