Manchester City Yaongeza Nguvu Kumsajili Anderson wa Nottingaham Forest

Mabingwa wa Ligi Kuu ya England Manchester City wanaripotiwa kuwa mbele katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson, huku wakizishinda klabu pinzani kama Manchester United na Arsenal.

Manchester City Yaongeza Nguvu Kumsajili Anderson wa Nottingaham ForestInaelezwa kuwa City wanatafuta kusajili kiungo mpya wa kati katika dirisha la usajili la majira ya joto, hasa ikizingatiwa uwezekano wa kuondoka kwa Bernardo Silva kutoka klabuni hapo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Anderson mwenye umri wa miaka 23 amekuwa mmoja wa wachezaji wanaotafutwa zaidi kwa sasa katika Ligi Kuu ya England, baada ya kuonyesha kiwango bora msimu huu licha ya timu yake ya Nottingham Forest kuwa katika hali ngumu ya ushindani.

Manchester City Yaongeza Nguvu Kumsajili Anderson wa Nottingaham Forest“Ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na uwezo wa kuleta mabadiliko uwanjani. Ndiyo maana klabu kubwa zinamfuatilia kwa karibu,” ilieleza moja ya vyanzo vya karibu na sakata hilo.

Ripoti zinaeleza kuwa Manchester City wako mstari wa mbele kukamilisha usajili huo, lakini ushindani bado upo mkali kutoka kwa Arsenal na Manchester United ambao pia wanahitaji huduma ya kiungo huyo wa kimataifa wa England.

Manchester City Yaongeza Nguvu Kumsajili Anderson wa Nottingaham Forest“Mbio bado hazijaisha. Kuna klabu kadhaa kubwa zinazoonyesha nia, hivyo uamuzi wa mwisho utategemea ofa na maono ya mchezaji,” kiliongeza chanzo hicho.

Manchester City Yaongeza Nguvu Kumsajili Anderson wa Nottingaham ForestInakadiriwa kuwa Nottingham Forest wanaweza kuhitaji ada ya takribani pauni milioni 100 ili kumuachia Anderson, jambo linaloweza kufanya usajili huo kuwa miongoni mwa dili kubwa zaidi msimu ujao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.