Kiungo wa muda mrefu wa Real Madrid, Dani Ceballos, anaripotiwa kuwa mbioni kuondoka klabuni hapo msimu huu wa kiangazi, akimaliza safari ya takribani miaka tisa ndani ya jiji la Madrid.
Ceballos mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Real Madrid mwaka 2017 akitokea Real Betis kwa ada inayokadiriwa kuwa euro milioni 18. Tangu hapo, ameichezea klabu hiyo mechi 214 na kufanikiwa kutwaa jumla ya mataji 15.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika kipindi chake cha uwepo Madrid, kiungo huyo pia aliwahi kutolewa kwa mkopo katika klabu ya Arsenal kati ya mwaka 2019 hadi 2021, ambapo alipata nafasi zaidi ya kucheza na kuonesha kiwango chake.
“Mkataba wake unaelekea ukingoni na kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka mwishoni mwa msimu,” ilieleza ripoti inayohusishwa na mwanahabari maarufu wa usajili Fabrizio Romano.
Msimu huu, Ceballos amepata dakika 810 pekee katika michezo 22, hali inayoashiria kupungua kwa nafasi yake ndani ya kikosi cha Real Madrid na kuongeza uwezekano wa kutafuta changamoto mpya.
Miongoni mwa vilabu vinavyotajwa kuwania saini yake ni Ajax, ambao wanapanga kufanya maboresho makubwa ya kikosi chao chini ya mkurugenzi wa ufundi Jordi Cruyff.
“Tunatafuta kuijenga upya timu ili kurejesha ushindani, na wachezaji wenye uzoefu kama Ceballos wanaweza kuwa sehemu ya mpango huo,” imeelezwa kutoka ndani ya Ajax, ambao kwa sasa wanashika nafasi ya tano kwenye ligi ya Eredivisie bila kutwaa taji kwa misimu minne mfululizo.

