Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani, Serge Gnabry, ametangaza kuwa hatoshiriki kwenye Kombe la Dunia la 2026 kutokana na jeraha la paja, akisema ndoto yake ya mashindano hayo imefikia mwisho.
Gnabry alithibitisha taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii, akieleza kuwa amepata majeraha ya Paja yatakayomuweka nje kwa muda mrefu, hatua iliyothibitishwa pia na klabu yake Bayern Munich.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Alisema “Siku chache zilizopita zimekuwa ngumu sana kuzichukulia. Msimu wa Bayern bado una mengi ya kupigania baada ya kutwaa ubingwa wa Bundesliga, lakini kwa upande wa ndoto ya Kombe la Dunia na Ujerumani, kwa bahati mbaya imeisha kwangu.”
Nyota huyo wa zamani wa Arsenal aliongeza “Kama taifa lote, nitakuwa nikiwashangilia vijana wetu kutoka nyumbani. Sasa ni wakati wa kuangazia uponyaji na kurejea vizuri kwa maandalizi ya msimu ujao.”
Kocha wa Ujerumani Julian Nagelsmann amekuwa akimtegemea sana Gnabry katika kikosi cha taifa, ambapo mshambuliaji huyo ameifungia Ujerumani mabao 26 katika mechi 59 alizocheza.
Taarifa hiyo ni pigo kubwa kwa timu ya taifa ya Ujerumani, ambao walikuwa wakimtegemea katika mashindano ya kimataifa, huku mashabiki wakisubiri kuona namna timu itakavyokabiliana na pengo lake.

