Jayrutty Yakabidhi Magari kwa Nyota Wapya Simba sc

Kampuni ya Jayrutty, ambayo ni mzabuni wa jezi za Simba sc, imekabidhi magari matano mapya kwa wachezaji watano wa timu hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, CPA Joseph Rwegasira. Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya kuthamini mchango wa wachezaji hao katika kuipa mafanikio klabu hiyo tangu walipo wasili kwenye klabu hiyo.

Jayrutty Yakabidhi Magari kwa Nyota Wapya Simba sc

Wachezaji waliokabidhiwa magari hayo ni viungo washambuliaji Libase Gueye, Jospin Inno Loemba na Anicet Aoura, pamoja na beki Ismaila Toure na golikipa Djibrilla Kassal. Makabidhiano hayo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi iliyotolewa kwa wachezaji hao kutokana na mchango wao ndani ya kikosi cha Simba.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Jayrutty Yakabidhi Magari kwa Nyota Wapya Simba sc

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba sc, Ahmed Ally amesema, “Wachezaji wa Simba SC ni wachezaji wakubwa ni mastaa pia hivyo tumewapa magari ili waendane na ukubwa wa klabu yetu. Tunataka wakatupe magoli na makombe hivyo tunataka wafurahie. Hatujawapa wachezaji magari kisa waliwatesa watu kule Amaan Complex, ila ni ukubwa wa klabu yetu.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.