Ikiwa ni muda mchache umepita tangu kiungo rasta wa Kizanzibar, Awesu Awesu, atambulishwe rasmi kama mchezaji mpya wa klabu ya Police Kenya FC, ameaza kugonga vichwa vya habari nchini humo na kutajwa kuwa huenda akawa staa mpya wa ligi hiyo.
Awesu kujiunga na timu hiyo ni hatua inayomfungulia ukurasa mpya katika safari yake ya soka la kulipwa nje ya nchi. Mara baada ya kutamba na klabu za hapa ndani kama Azam FC, KMC na Simba ambayo imemtoa kwa mkopo.

Awesu ametua katika klabu hiyo ya Ligi Kuu Kenya kwa mkataba wa miezi sita, makubaliano yanayolenga kuongeza ushindani kikosini pamoja na kuimarisha safu ya kiungo kuelekea michezo ya nusu ya pili ya msimu.
Kupitia taarifa rasmi za klabu, Awesu amepewa jezi namba 33, namba ambayo ataitumia katika mechi zote za mashindano ya ndani na mengineyo atakayoshiriki Police Kenya FC msimu huu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Ujio wa nyota huyo umeibua matumaini makubwa kwa mashabiki wa Police Kenya FC, wakiamini uzoefu wake wa kimataifa na uwezo wake wa kukaba, kupiga pasi sahihi na kusoma mchezo utaongeza ubora mkubwa ndani ya kikosi.


