AWESU AWESU NI MALI YA SIMBA

Aliyekua kiungo wa klabu ya KMC Awesu Awesu inaelezwa usajili wake wa kujiunga na wekundu wa msimbazi klabu ya Simba umekamilika leo ambapo ndo mwisho wa dirisha la usajili.

Klabu ya Simba iliripotiwa kumsajili kiungo Awesu Awesu kinyume na taratibu jambo ambalo klabu ya KMC ilifikisha shauri hilo TFF na shirikisho kuamuru mchezjai huyo arudi klabuni yake ya KMC au klabu ya Simba ifate taratibu kumpata kiungo huyo  kutoka visiwani Zanzibar.simbaTaarifa zilizotoka jioni hii ni kua klabu ya Simba imefikia makubaliano na klabu ya KMC kuhakikisha wanapata saini ya mchezaji huyo fundi ambaye amewahi kupita klabu ya Azam Fc, Hivo vilabu vyote viwili vimekaa mezani na kufikia muafaka na sasa rasmi kiungo huyo ni mali ya wekundu wa msimbazi.

Dau ambalo limetumika kumsajili kiungo Awesu Awesu kutoka klabu ya KMC halijawekwa wazi kua ni kiasi gani cha pesa kimetumika, Lakini taarifa za uhakika ni kua kiungo huyo ataitumikia klabu ya Simba kuelekea msimu ujao wa 2024/25 akiwa na mkataba wa miaka miwili ndani ya viunga vya msimbazi.

Acha ujumbe