Ten Hag: De Ligt na Mazraoui Watakuepo Dhiidi ya Fulham Kesho

Kocha wa klabu ya Manchester Erik Ten Hag ameweka wazi kua wachezaji wawili ambao wametambulishwa kwenye kikosi hicho Mathijjs De Ligt na Noussair Mazraoui watakua sehemu ya timu kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Fulham.

Manchester United watafungua pazia la ligi kuu ya Uingereza kesho watakapocheza dhidi ya Fulham katika dimba la Old Trafford, Huku wachezaji wawili ambao wamesajiliwa ndani ya timu hiyo wakiwa sehmu ya kikosi cha kesho kutokana na maelezo ya kocha Ten Hag kuelekea mchezo huo wa ufunguzi.ten hagKocha huyo ameeleza hayo huku akigusia pia suala la beki Harry Maguire kua fiti kucheza mchezo wa kesho dhidi ya Fulham ambapo Luke Shaw yeye ndo anatarajiwa kukosekana michezo kadhaa ya mwanzoni mwa msimu, Kuwepo kwenye kikosi cha kesho kwa wachezaji walifanya mazoezi na timu kwa siku mbili tu inaonesha kwa namna klabu hiyo inasumbuliwa na majeraha.

Manchester United mpaka sasa ina wachezaji watatu wa eneo la ulinzi ambao wanne majeraha ambao ni Leny Yoro, Victor Lindelof, Tyrell Malacia, pamoja na Luke Shaw, Hii ni moja ya sababu mabazo zimemfanya kocha Ten Hag kuwaweka kwenye kikosi cha kesho wachezaji De Ligt na Mazraoui.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.