Ten Hag: Rashford Hajapata Majeraha makubwa

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesema kua majeraha aliyoyapata mshambuliaji wa klabu hiyo Marcus Rashford sio makubwa sana.

Rashford alipata majeraha katika mchezo wa jana wa kirafiki dhidi ya klabu ya Real Betis ambapo ilipelekea kushindwa kumaliza mchezo, Lakini kocha Ten Hag ameongea na kusema majeraha hayo sio makubwa sana hali ambayo imeshusha presha kidogo kwa mashabiki wa klabu ya Man United.ten hagManchester United imekua ikiandamwa na majeraha tangu msimu uliomalizika ambapo mpaka sasa wameshapata majeraha ya wachezaji wanne ndani ya kikosi hicho, Lakini kocha wa klabu hiyo ameweka wazi kua mipango ya klabu hiyo haitabadilishwa na majeraha ambayo wamekua wakiyapata kwakua majeraha ni jambo lisiloepukika.

Kocha Erik Ten Hag ameendelea kusisitiza kua ana imani kubwa na Rashford na ana uwezo wa kurejea kwenye ubora wake ambao alikua nao misimu miwili nyuma ambapo alifunga mabao 30, Kocha huyo anaamini anaweza kufanya hivo kwakua ana uwezo mkubwa na wanachofanya kwasasa ni kumpa ushirikiano wa karibu kuhakiisha anapona majeraha yake.

Acha ujumbe