Girona Yaendelea Kuvunjwa

Klabu ya Girona imeendelea kuvunjwa kuelekea msimu ujao ambapo beki wake wa kulia raia wa kimataifa wa Brazil Yan Couto amejiunga na klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani.

Baada ya kua na msimu bora sana jwenye ligi kuu ya Hispania na kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo klabu ya Girona inakutana na wakati mgumu wa kuwabakiza wachezaji wake nyota ambao walifanikisha wao kufanya vizuri msimu wa 2023/24, Kwani wachezaji wake muhimu wanaendelea kutimka klabuni hapo.gironaKlabu ya Borussia Dortmund imefanikiwa kumsajili beki wa kimataifa wa Brazil ambaye alikua anakipiga klabu ya Girona msimu uliomalizika na akiwa sehemu ya mafanikio ya klabu hiyo Yan Couto, Dortmund wamefanikiwa kulipa kiasi cha Euro milioni 25 kwa klabu ya Manchester City ambao ndio wamiliki halali wa mchezaji huyo.

Mchezaji Yan Couto alikua mchezaji muhimu ndani ya klabu ya Girona licha ya yeye kuwepo klabuni hapo kwa mkopo akitokea klabu ya Manchester City, Lakini klabu hiyo kutoka nchini Hispania imepata pigo kwakua walikua na mkakati wa kuendelea kumtumia mchezaji huyo lakini Dortmund wamewazidi dau na kufanikiwa kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil.

Acha ujumbe