Kibu Denis Ajiunga na Kambi ya Simba

Mshambuliaji wa klabu ya Simba  Kibu Denis amerejea nchini Tanzania na amejiunga na kambi ya timu hiyo kuelekea siku ya Simba Day ambayo itafanyika siku ya Jumamosi Agosti 4.

Kibu Denis ambaye aliacha taharuki siku kadhaa nyuma baada ya kushindwa kuripoti kwenye kambi ya klabu hiyo ambayo ilikua nchini Misri kujiandaa na msimu mpya, Huku tasarifa zikieleza alienda nchini Norway kwajili ya kufanya majaribio ya kujiunga na moja ya timu zilizokua nchini humo.kibu denisMshambuliaji huyo ameonekana katika uwanja wa Benjamin Mkapa mapema leo akifanya mazoezi na wenzake kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya APR ya nchini Rwanda, Hii inaonesha mchezaji huyo ameshamilizana na uongozi wa klabu ya Simba ambao ulikua unadaiwa kumpa adhabu mchezaji huyo kwani aliondoka kwenye timu hiyo na kutimkia nchini Norway pasipo idhidi ya klabu yake.

Mchezaji Kibu Denis ni wazi sasa atakua sehemu ya kikosi cha Simba kuelekea msimu ujao tofauti na ilivyotarajiwa na wengi ambapo ilidhaniwa angepewa adhabu kubwa klabuni hapo baada ya kukiuka taratibu za kimkataba, Lakini hali ilivyo mpaka sasa Wekundu wa msimbazi wanaonekana kumsamehe mchezaji huyo.

Acha ujumbe