Ten Hag Akiri Kumaliza Tofauti na Sancho

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag ameweka wazi kumaliza matatizo yake na winga wa klabu hiyo Jadon Sancho ambayo walikua nayo kwa kipindi cha miezi tisa nyuma.

Ten Hag amefunguka leo mbele ya waandishi wa habari kua amemaliza tofauti zake na winga huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye msimu uliomalizika alikua anakipiga kwa mkopo klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani, Lakini wiki iliyopita alionekana kwenye mazoezi ya klabu hiyo jambo lilionesha tofauti zimemalizika baina ya wawili hao.ten hag“Manchester United wanahitaji wachezaji wazuri na Jadon ni mchezaji mzuri.”

“Tumeweka mstari huo na tunaendelea mbele, ndiyo.”ameyazungumza hayo kocha huyo ambaye walikua kwenye mvutano na Sancho kwa muda mrefu.

Jadon Sancho tayari alishawekwa sokoni kwenye klabu hiyo lakini kutokana hali inayoendelea klabuni hapo kwasasa kwa yeye kumaliza tofauti na kocha Ten Hag inaweza kubadilisha maamuzi ya uongozi wa klabu, Lakini itategemea zaidi ubora ambao atauonesha mchezaji huyo ndani ya klabu ya Man United.

Acha ujumbe