Pa Omar Jobe Atemwa Simba

Zile “Thank You” ndani ya klabu ya Simba hazijaisha na mapema leo saa tisa kamili Alasiri imetangaza kumuacha aliyekua mshambuliaji wake Pa Omar Jobe.

Pa Omar Jobe ametemwa ndani ya klabu ya Simba baada ya kudumu klabuni hapo kwa miezi sita kwani mshambuliaji huyo alisajiliwa ndani ya viunga vya Msimbazi katika dirisha dogo la mwezi Januari, Lakini kutokana na kutokufika matarajio ametemwa na klabu hiyo.pa omar jobeMoja ya wachezaji ambao mazungumzo yake na klabu ya Simba yamekua ya muda mrefu kwakua walikua wanashindwa kufikia muafaka kutokana na madai ambayo angetakiwa kulipwa mchezaji huyo kama angevunjiwa mkataba, Lakini leo klabu hiyo imeamua kuachana nae ni wazi wamekubali kumvunjia mkataba mchezaji huyo na kumlipa stahiki zake.

Mshambuliaji Pa Omar Jobe sasa ni rasmi anaungana na lile kundi la wachezaji waliopewa mkono wa kwaheri na Simba kuelekea msimu ujao, Ambapo klabu hiyo inaelezwa kuhitaji kutengeneza timu mpya ambayo itarudisha heshima ya mnyama na wachezaji walioachwa walionekana kama hawaweza kuwapeleka wanapotaka.

Acha ujumbe